Filename ICWEA-HIV-Criminalizing-Policy-Brief-Swahili-1.pdf
Filesize 2.86 MB
Version pdf
Date added August 11, 2020
Downloaded 356 times
Category Policy Brief
slide_template default

kuhusu kiasi cha faulu au ukosefu wa sera za kitaifa au za kimataifa, masharti na sheria kuhusu
suluhisho la Ukimwi. Huibuka kataika muktadha wa Ukimwi na haki za kibinadamu na kuandaa
miradi bora ya kukabili Ukimwi. Mkabala bora ni pale unapoweza kutimiza malengo ya jumuiya
ya kimataifa ya kupima, kukinga na kutoa matibabu. Mkabala wa Uganda dhidi ya Ukimwi
umekuwa wenye uwazi, kuwajibika kwa pamoja, mchango mkubwa wa viongozi wa kisiasa na
ushirikiano na mashirika ya nchini na ya kimataifa. Lakini, katika mwaka 2014, nchi ya Uganda
ilipitisha sheria ya Kudhibiti na Kukinga Ukimwi. Sehemu III, aya 43 ya sheria hiyo inataja kwamba
“yeyote atakayedhamiria au kuwa na nia ya kusambaza Ukimwi kwa mtu mwingine atakuwa
ametenda kosa la jinai na atahukumiwa kifungo kinachotimia miaka 10”. Tamko hili linachukulia
kwamba mtu huwa tayari anajua kuwa ama ana Ukimwi au hana, ndipo “adhamirie” and “awe na
nia ya” kusambaza Ukimwi. Lakini, ushahidi wa utati uliopo unaonyesha kwamba kitendo kama
hiki cha kuchukua hatua za kisheria kinaweza kutia watu hofu wasijitokeze kwenda kupimwa
Ukimwi na kupata huduma nyinginezo husika.