Filename APN-ICWEA-Policy-Brief-Swahili-1.pdf
Filesize 2.63 MB
Version pdf
Date added August 11, 2020
Downloaded 354 times
Category Policy Brief, Position Paper
slide_template default

Kusaidiwa kujulisha mchumba umekuwa mkabala muhimu unaotumiwa na maafisa wa
afya katika kutibu magonjwa yanayosambazwa kutoka mtu mmoja hadi mwingine kwa
miongo kadha, mkiwemo mipango inayolenga magonjwa ya zinaa na kifua kikuu (TB).
Mikabala ya kuwajulisha wachumba hali yao ya afya imeonekana kuwa inafaulu katika
kupima na kutibu magonjwa ya zinaa na kuzuia kuambukizwa tena. Vile vile, kuendelea
kufuatilia watu wenye uhusiano na wagonjwa na vipimo vya kujitolea kwa jamaa za
wagonjwa wa TB ni njia bora na iliyo mwafaka ambayo imetumika na ikafaulu kwenye
jumuiya zenye kiasi kikubwa cha wagonjwa wa Ukimwi na TB. Kufikia mwisho wa mwaka
2015, ilikadiriwa kwamba zaidi ya watu miliyoni 36 duniani kote walikuwa na Ukimwi, na
asilimia 40 kutoka idadi hiyo walikuwa hawajapimwa. Ili kuziba pengo hili na kutimiza
malengo ya vipimo na matibabu ya shirika la UNAIDS (malengo ya 90:90:90), mikakati
mipya ilihitajika ili kuwezesha vipimo vingi sana na vyenye kiwago bora. Mkakati
kusaidiwa kujulisha mchumba unaweza kusababisha ongezeko la vipimo wakati pia watu
wenye Ukimwi ambao hawajapimwa watajulikana.